MAKANISA Yamekuwa Dili..Mrembo Irene Uwoya Atangaza Kuanzisha Kanisa lake

0 comments
 
Msanii wa filamu Irene Uwoya amesema kuwa ana mpango wa kuwa Mchungaji pamoja na kumiliki kanisa lake yeye mwenyewe siku za usoni na kwamba anamuomba Mungu kila siku aweze kutimiza ndoto hizo.


Kauli hii imetoka kinywani mwa msanii huyo pindi alipokuwa akijibu maswali mubashara aliyokuwa anaulizwa na mashabiki zake kupitia katika ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipindi cha Kikaangoni


"Nina ndoto ya kuwa mchungaji na kila siku huwa nina muomba Mungu anifanikishie suala hilo niweze kutimiza japokuwa sasa hivi bado nipo katika changamoto kubwa ila natumai ndoto zangu zitatimia. Natamani kuwa pastor ambaye ni mwalimu, niwafundishe watu Mungu anataka nini, lakini sitaki kuanzisha kanisa kama biashara, sitaki kucheza na Mungu, ndiyo maana najipanga kwanza sitaki kukurupuka, nataka niwafundishe watu Mungu anataka nini, na jinsi ya kumuomba Mungu". Alisema Uwoya


Uwoya pia amefunguka na kueleza kuwa kazi yake ya sanaa huwa inamtesa kiimani jambo ambalo linamfanya kila siku akiamka awe anatubu kwa ajili ya mambo anayoyafanya akiwa katika kazi zake za uigizaji .


Amesema katika tasnia ya uigizaji mara nyingi huwa wanaongea uongo na hata mambo mengi wanayoyafanya kufikisha ujumbe huwa ni vitu ambavyo havimpendezi Mungu.


"Mimi nina hofu ya Mungu sana pia napenda kusali linapokuja suala la kazi yangu ukweli naona kama inanisumbua imani yangu kwa sababu katika uigizaji mambo mengi tunayoyafanya siyo ya kumpndeza Mungu lakini ndiyo kazi sasa, kila siku asubuhi nikiamka huwa inabidi kumuomba msamaha mungu wangu ndiyo niendelee na kazi". Amesema Irene Uwoya.


Kwa waliotaka kujua kama Irene anatumia dawa za kulevya, amewajibu kuwa hatumii dawa za kulevya na hajawahi kutumia kwa kuwa ni mkristo na dini yake hairuhusu kutumia dawa za kulevya wala kushiriki katika ndoa za jinsia moja lakini pombe anakunywa


"Situmii dawa za kulevya lakini nakunywa bia, dini yangu haizuii kunywa, nina uwezo wa kumaliza hata kreti nzima, hata mapadre kwenye dini yetu wanakunywa, lakini hairuhusiwi kulewa"


Pia amefunguka kuhusu mapenzi yake ya kuvaa nguo fupi, ambapo amesema anapeda nguo fupi, kwa kuwa ana mzio 'allergy' na nguo ndefu, hivyo hawezi kuvaa nguo ndefu.

Read More »

Mbowe Afunguka ya Moyoni Baada ya Jana Kutajwa na Makonda,Afichua Njama Hizi za CCM kwa Chama Chake..!!!

0 comments
     

Muda mfupi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwaita polisi kuhojiwa kwa tuhuma mbalimbali, baadhi ya walioitwa wamelaani hatua hiyo wakisema inalenga kuwachafulia majina na heshima mbele ya jamii.

Miongoni mwa waliotwa ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ambaye amezungumza na kueleza kutofurahishwa na hatua hiyo.

Mbowe aliyekuwa safarini kwenda bungeni Dodoma, alisema ameshangazwa kutuhumiwa kwa jambo asilolijua.

“Kama amemtaja mbunge wa Hai anajulikana ni mmoja, hata kama asingesema Freeman, Mbunge wa Hai anajulikana ni Freeman Mbowe.

“The only thing (kitu pekee) ninaweza kusema nchi haiendeshwi hivyo. Yametajwa majina mengi ambayo sijui Makonda ana evidence (ushahidi) gani!

“Anasema tukiwaita tukiridhika na maelezo yao tutawaachia. Huwezi kusema tu, yaani kwa kusema ni Mbowe... mimi ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, mimi ni mbunge, mimi ni mzazi, nina wanachama, maaskofu, mapadri, mashehe na viongozi mbalimbali.

“Unapokuwa unamhusisha kiongozi na ‘drug trafficking au drug business’ (usafirishaji wa dawa au biashara ya dawa za kulevya), sijui ana ushahidi gani hadi akanihusisha na jambo hilo, mimi sielewi, kwa hivyo siwezi kusema kwa kitu ambacho sielewi,”alisisitiza Mbowe.

Mbowe aliendelea kusema kuwa kesi za dawa za kulevya hazina dhamana, hivyo alimtaka Makonda awe na ushahidi wa kutosha anapowataja watuhumiwa.

“Tuache habari ya kuitwa, wewe umepata tuhuma, hujafanya uchunguzi, hakuna mtu aliye juu ya sheria, lakini unatakiwa kufanya uchunguzi ili ukimkamata mtu unamshtaki, siyo unataja mtu unachafua hadhi yake. Halafu ukija kusema hatuna ushahidi juu yako umeshaharibu jina lake,” alisema na kuongeza:

“Mimi sijui kama jeshi la polisi linafanya kazi hii au ni Makonda amejipa kazi ya kuwa mpelelezi. Au labda yeye kwa kuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ndiyo amejipa kazi ya kutaja majina kwenye mambo yenye kashfa kama haya? Sielewi. This is very wrong precedence (Hii ni rejea mbaya) kwa utawala wa sheria.”

Mbowe alisema inawezekana ni mikakati ya Serikali kuendelea kukandamiza upinzani kwa kuwakamata viongozi wake.

“Sijui kama kuna watu wanaolengwa, lakini tumeona viongozi wetu wanakamatwa hawapewi dhamana, (Tundu) Lissu amekamatwa, (Godbless) Lema amekamatwa ... mtu anakaa miezi minne, kwa hiyo wanaweza kufanya lolote. Inawezekana ni mkakati wa kutesa wapinzani. Wamenitafuta kwenye biashara wameona haitoshi... sina uhakika lakini sioni kama wana nia njema na sisi,” alisema Mbowe.


Alipoulizwa kama ataitikia wito wa Makonda, Mbowe alisema bado anawasiliana na wanasheria wake kabla ya kuchukua hatua.

Read More »

Kutoka Mahakamni..Ombi la Serikali la Kutaka Lissu Anyimwe Dhamana Latupwa,Lissu Akipewa Dhamana ya Milioni 20

0 comments
                                 

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka manne ya uchochezi.

Wakili wa Serikali Kishenyi Mutalemwa  aliwasilisha maombi ya kupinga dhamana yaTundu Lissu kwa madai kwamba   amekuwa na mwenendo unaohatarisha amani si tu kwa wanajamii, bali hata kwake mwenyewe kwa kuendelea kutoa maneno ya uchochezi.


Hakimu Huruma Shaidi, ametupilia mbali ombi hilo la serikali na kumpa  Tundu Lissu dhamana ya sh. Milioni 20

Read More »

WAZIRI Aipiga Stop EWURA Kupandisha Bei ya Umeme

0 comments
Waziri wa nishati na madini, Sospeter Muhongo ameipiga 'Stop' EWURA kupandisha bei ya umeme mpaka serikali itapopokea na kutathmini bei mpya kwa umakini.


Jana EWURA ilatangaza ongezeko la bei ya umeme kuanzia Januari mosi, 2017.

Read More »

WASHITAKIWA Wanne Mauaji wa Dr. Mvungi Waachiwa Huru

0 comments
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru washitakiwa wanne kati ya 10 waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka ya mauaji ya bila  kukusudia ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi.

Washitakiwa walioachiwa ni Masunga Makenza (40), mkazi wa Tabata Darajani, Zacharia Msese (33), Ahmad Kitabu (30) mkazi wa Mwananyamala na John Mayunga (56).

Waliachiwa kwa mujibu wa Kifungu Namba 91 Kifungu kidogo cha kwanza cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA). Wakili wa Serikali, Pamela Shinyambala alidai mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba kuwa upande wa mashitaka umeshasajili jalada hilo Mahakama Kuu.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mshitaka Nchini (DPP), hakuwa na nia ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa hao kwa mujibu wa kifungu hicho. Awali, Shinyambala alidai kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutolewa maelezo ya mashahidi baada ya upelelezi wa kesi hiyo kukamilika.

Hakimu Simba alisema anawaachia washitakiwa hao, kama walivyoomba upande wa mashitaka. Alisema kwamba washitakiwa sita, ndio watakaosomewa maelezo hayo ya mashahidi.

Washitakiwa hao ni Longishu Losingo (29), Paulo Mdonondo (30) mkazi wa Tabata Darajani, Mianda Mlewa (40) Mkazi wa Vingunguti, Juma Kangungu (29) mkazi wa Vingunguti, Msungwa Matonya (30), mkazi wa Vingunguti na Masenga Mateu.

Hata hivyo, Hakimu Simba aliutaka upande wa mashitaka, kuhakikisha kwamba wanaleta cheti cha kifo cha mshitakiwa wa kwanza, Chibago Magozi (32), mfanyabiashara mkazi wa Vingunguti Machinjioni.

Pia alieleza kuwa kesi hiyo ikienda mahakama kuu, bila ya kupelekwa mahakamani hapo cheti cha kifo, itakwama kwa kuwa hawawezi kusoma maelezo hayo hadi kwa mtu aliyekufa.

Aliwataka kuhakikisha katika tarehe ijayo ambapo washitakiwa sita watasomewa maelezo, wawe wamewasilisha cheti cha kifo.

Hata hivyo, Wakili Shinyambala alikubaliana na maelezo hayo na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea washitakiwa waliobaki maelezo ya mashahidi. Kesi imepangwa Januari 10,

Read More »

HOJA Sita za rufaa ya Mbunge Lema Kusikilizwa leo

0 comments
 
Hoja sita za mawakili wa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kupinga kunyimwa dhamana zinatarajiwa kusikilizwa leo mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Salma Maghimbi.

 Wakili Sheck Mfinanga anayemwakilisha Lema alisema waliwasilisha hoja hizo za rufaa kupinga uamuzi wa kunyimwa dhamana mteja wao.

 Lema aliyekamatwa Novemba 2, akiwa mjini Dodoma, tangu wakati huo anashikiliwa kwenye Gereza Kuu la Kisongo jijini Arusha ambako amekaa kwa siku 56.

 Baada ya kukamatwa na kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Lema alipewa dhamana na Hakimu Mkazi Desdery Kamugisha katika kesi namba 440 na 441/2016 akidaiwa kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli.

 Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) alikata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama kumpa dhamana mbunge huyo.

Mawakali wa Lema nao walikata rufaa kupinga mteja wao kunyimwa dhamana ambayo imepangwa kusikilizwa leo baada ya kukwama kwa muda mrefu kutokana na kuwapo pingamizi za kisheria zilizowasilishwa na upande wa Jamhuri.

Read More »

TUNDU Lissu Akamatwa na Jeshi la Polisi

0 comments
 
TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam

“Nashikiliwa na polisi hapa Kituo Kikuu kutokana na ile press conference (mkutano na waandishi wa habari) kuhusu kupotea kwa Ben Saanane,” alimweleza mwandishi wa habari hii kupitia simu leo.

Mwandishi alimtafuta Lissu kutaka kujua baadhi ya mambo, ndipo alipopokea simu na kueleza hivyo. Hakuna taarifa zaidi mpaka sasa.

Saanane ambaye ni Msaidizi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa-Freeman Mbowe alipotea ghafla takribani mwezi mmoja sasa na hajulikani alipo.

Wafuasi wa CHADEMA wamekuwa wakimsaka kiongozi huyo bila mafanikio yoyote jambo ambalo limeendelea kuzua hofu kama yu hai ama ameuawa.

Tarehe 14 Desemba mwaka huu, Lissu alizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam akiomba vyombo vya ulinzi kusaidia kupatikana kwa kiongozi huyo.

Chanzo: Mwanahalisi

Read More »